TEHRAN
15 Februari 2005Matangazo
Watu 60 wamekufa na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa baada ya kutokea moto mkubwa katika msikiti mmoja uliojaa waumini mjini Tehran,Iran.Polisi wamesema mto huo ulizuka baada ya waumini kuingia msikitini kwa ajili ya ibada,ikiwa zimesalia siku chache kabla Waislamu wa madhehebu ya Shia hawajaadhimisha sikukuu yao ya Ashura.
Taarifa za vyombo vya habari vya Iran zimeeleza kuwa moto huo umesababishwa na chombo cha kupashia joto ama heater kilichoingizwa msikitini humo kwa ajili ya kuwapunguzia makali ya baridi waumini.