TEHRAN:Iran yalitangaza jeshi la Marekani na CIA kuwa makundi ya kigaidi
30 Septemba 2007Matangazo
Bunge la Iran hapo jana liliidhinisha azimio la kulitangaza jeshi la Marekani pamoja na idara ya ujasusi ya nchi hiyo CIA kuwa ni makundi ya kigaidi.
Hatua hiyo inaonekana kulipa kisasi, kidiplomasia kufuatia bunge la seneti la Marekani kupitisha azimio linalotaka serikali ya nchi hiyo kulitangaza jeshi la kimapinduzi la Iran kuwa kundi la kigaidi.
Taarifa iliyotolewa na wabunge 215 wa bunge la Iran imesema kuwa idara ya ujasusi ya Marekani na jeshi la kivamizi la nchi hiyo na makundi la kigaidi.
Bunge hilo limesema kuwa vyombo hivyo viwili vilihusika na ulipuaji wa bomu la nukilia katika vita kuu ya pili ya dunia nchini Japan, pamoja na kuzivamia Iraq na Afghanistan.