1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Iran yaondosha vizuizi vya Umoja wa Mataifa kwenye mtambo wake wa Nuklia wa Isfahan

10 Agosti 2005

Iran imeanza kuviondosha vizuizi vilivyosalia kwenye mtambo wake wa nuklia wa Isfahan vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa ili kuiwezesha kufanya kazi kikamilifu.

Hatua ya Iran imekuja huku shirika la Atomiki duniani la Umoja wa Mataifa likiuhairisha mkutano wake juu ya Iran uliokuwa ufanyike leo.

Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo mkutano huo huenda ukafanyika kesho.

Shirika hilo linataka kuishawishi Iran kuachana na mpango wake wa shughuli za kinuklia.

Umoja wa Mataifa uliweka vizuizi kwenye maeneo mepesi ya mtambo huo mnamo mwezi Novemba, baada ya Iran kukubali kukomesha shughuli zake zote za kutengeneza mafuta ya Nuklia kama sehemu ya maafikiano baina ya nchi hiyo na Uingereza Ujerumani na Ufaransa.

Hata hivyo rais mpya wa Iran Mahmoud Abdinejad ameitetea hatua ya serikali ya kuanzisha tena shughuli zake za kinuklia katika mtambo wa Isfahan huku akisema serikali yake bado inataka kuendelea na mazungumzo na Umoja wa Ulaya.

Mtambo wa Isfahana unaweza kuyabadili madini ya Uranium na kuwa gesi inayoweza baadae kurutubishwa na kuwa mafuta ya kutengeneza bomu jambo linalohofiwa na Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW