TEHRAN:Iran yasema iko tayari kushirikiana na IAEA
28 Agosti 2007Matangazo
Maafisa wa Iran wamesema wametoa habari zilizohitajika na shirika la Umoja wa mataifa la kudhibiti technologia ya nishati ya Nukilia IAEA kuhisiana na mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium ambao unadaiwa na Marekani kuwa unatumiwa kutengeneza silaha za Kinuklia
Ingawa Iran imekanusha madai hayo ya Marekani imeahidi kwa upande mwingine kushirikiana na shirika hilo la IAEA na kuchapisha ratiba ya kutoa habati nyingine nyeti kuhusu shughuli zake za kinuklia.
Msemaji wa shirika la IAEA hata hivyo amekataa kuzungumzia chochote kuhusiana na hali hii.