TEHRAN.Iran yazindua awamu mpya ya maji
26 Agosti 2006Matangazo
Rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran amezindua awamu mpya ya mpango wa maji katika eneo la Arak.
Mpango huo unatarajiwa kupeleka kiwango cha maji mengi katika sehemu ya utafiti ambayo bado linaendelea kujengwa.
Maji hayo huenda yakawezesha kuundwa kwa madini ya Plutonium yanayohitajika kutengenezea bomu la atomiki.
Hii ni hatua mpya katika mpango wa nuklia wa Iran ambao nchi za magharibi zinashuku kuwa nchi hiyo ina lengo la kutengeneza silaha za atomiki.
Lakini Iran imekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya kawaida.