TEHRAN:Mkuu wa IAEA azisuta Marekani na washirika wake juu ya mpango wa Nuklia wa Iran
29 Oktoba 2007Matangazo
Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti Technologia ya Nuklia IAEA Mohammed El Baradei amesema hakuna ushahidi kwamba Iran inatengeneza silaha za Kinuklia.Akizungumza na Kituo cha Televisheni cha Marekani CNN El Baradei amesema ikiwa Iran inatengeneza silaha hizo za maangamizi basi ina miaka kadhaa kufikia hatua hiyo.Aidha mkuu huyo wa shirika la IAEA ameikosoa Marekani kwa kulipanua suala hilo.Pia amesema ni bora kwa kila mmoja kuiga mfano wa Korea Kaskazini wa kuharibu vinu vya Kinuklia.