1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran:Mkuu wa siasa za kigeni wa Umoja wa Ulaya akabidhi mapendekezo ya madola makuu kwa Iran.

6 Juni 2006

Mkuu wa siasa za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, ameikabidhi Iran mapendekezo yanayokusudia kuishawishi nchi hiyo isitishe harakati za kuwa na nishati ya kinyukliya. Mapendekezo hayo yalitayarishwa na Ujerumani, Uengereza na Ufaranbsa na yanaungwa mkono na Marekani, Russia na Uchina. Mkuu wa Iran juu ya mashauriano ya masuala ya kinyukliya, Ali Larijani, amesema nchi yake itatoa majibu baada ya kuyachunguza mapendekezo hayo ya kimataifa yanayohusu vivutio vya kibiashara, teknolojia na maingiliano ya kibalozi. Mapendekezo hayo yametolewa kwa sharti kwamba Iran isitishe shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium ambayo yanaweza kutengeneza silaha za kinyukliya. Pindi Iran haitayakubali mapendekezo hayo, basi hapo tena itakabiliwa na hatua kali kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikiwa pamoja na uwezekano wa kuwekewa vikwazo.

Javier aliwaambia waandishi wa habari mjini Tehran:

+Msimamo wa mwanzo wa Iran haujatolewa, lakini tunatumai sana kwamba mapendekezo haya yatavutia na itakua uzuri kwa Wa-Irani kuyazingatia sana. Ikiwa watasema wanakusudia kikweli kuzalisha nishati, na ikiwa watayakataa huenda mara nyingine hiyo ikawa ni ishara wazi kwamba wanatafuta kurutubisha Uranium kwa ajili ya silaha za kinyukliya, jambo ambalo kwetu sisi, nchi za Ulaya na sehemu kubwa ya jamii ya Kimataifa, itakuwa ni hatari sana.+

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW