1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Rais wa Iran asema yuko tayari kushirikiana na Iraq juu ya usalama

9 Agosti 2007

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amesema anamatumaini mazuri juu ya hatma ya Iraq na kwamba nchi hizo mbili Iran na Iraq kwa pamoja zinajukumu la la kuweka amani na usalama katika eneo hilo. Rais huyo wa Iran alisema hayo wakati wa mkutano wake na waziri mkuu wa Iraq Nouri al Maliki mjini Tehran.

Waziri mkuu wa Iraq pia alipata hakikisho kutoka kwa makamu wa kwanza wa r ais wa Iran Parviz Davoudi kwamba Iran inafanya kila iwezalo kuimarisha hali ya usalama nchini Iraq.

Ziara ya waziri mkuu Nouri a la Maliki nchini Iran imetokea siku mbili baada ya kamati ya maafisa wa Iraq , Iran na Marekani kuwa na mazungumzo mjini Baghdad juu ya kuimarisha ushirikiano wa juhudi za kuleta usalama Iraq.