Tel Aviv. Chama cha Labour kupata kiongozi mpya.
29 Mei 2007Chama cha Labour nchini Israel kinaonekana kuwa kitapata kiongozi mpya baada ya waziri wa ulinzi Amir Peretz kushika nafasi ya tatu katika uchaguzi uliofanyika jana Jumatatu.
Hata hivyo , uchaguzi huo umeshindwa kumpata mshindi wa wazi.
Matokeo ya hivi karibuni yamepunguza wagombea hadi kwa waziri mkuu wa zamani Ehud Barak pamoja na mwanasiasa mpya Ami Ayalon, lakini hakuna mtu aliyepata wingi wa asilimia 40 unaohitajika kupata ushindi wa moja kwa moja , na kusababisha kufanyika uchaguzi wa duru ya pili hapo Juni 12.
Chama cha Labour ni mshirika mkubwa wa chama cha waziri mkuu Ehud Olmert katika serikali ya mseto inayoongozwa na chama chake cha Kadima cha mrengo wa kati.
Iwapo kiongozi huyo mpya atakitoa chama cha Labour katika serikali ya mseto , huenda ukaitishwa uchaguzi mkuu.