1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Viongozi kukutana juu ya suala la amani kati ya Palestina na Israel

7 Machi 2005

Viongozi wa ngazi za juu wa Israel na Palestina wanapanga kukutana kwa mara nyingine.

Duru zimearifu kuwa rais wa Palestina Mahmoud Abbas na waziri wa Usalama wa Isarel Shaoul Mofaz wanatarajia kukutana hivi karibuni kuzungumzia upya mpango wa amani.

Mkutano huo utakuwa wa kwanza kufanyika tangu kutokea kwa shambulio la kujitoa muhanga lilifanywa na mpalestina mmoja katika mji wa Tel Aviv mwishoni mwa mwezi uliopita. Hii leo wapalestina waliokuwa na bunduki waliwajeruhi waisrael wawili katika mji wa Hebron magharibi mwa ukingo wa gaza.

Hapo jana wakuu wa usalama wa Israel na Palestina walikutana katika kile kilichoonekana kuwa hatua ya kuondosha uhasama baada ya shambmulio hilo la Tel Aviv ambapo waisrael watano waliuwawa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW