1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Walowezi wampinga Sharon

12 Januari 2004
Maelfu ya walowezi wa kiyahudi waliandamana kwa wingi hapo jana mjini Tel Aviv kupinga majaribio ya Waziri Mkuu Ariel SHARON ya kuvunja baadhi ya makazi yao kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa amani na Wapalastina. Bwana SHARON ameonya uwezekano wa kuvunjika majadiliano na Wapalastina iwapo atashindwa kuvunja makazi hayo, jambo ambalo linapingwa na walowezi pamoja na baadhi ya wasaidizi wake serikalini. Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Palastina, Ahmed QOREI amerejea mwito wake kwa Israili kuiomba iachane na mpango wa kujenga ukuta wa usalama kati yake na Ukingo wa magharibi wa Mto Jordan. Bwan QOREI ameomba Marekani, Urusi, nchi za Ulaya na Umoja wa Mataifa, ambao ndio wanadhamini wa Mpango Mpya wa amani ya Mashariki ya kati, kuishawishi Israili kuhusu suala hilo akionya kuwa ukuta huo ni kikwazo kikubwa kwa amani ya Mashariki ya kati. Israili inadai kuwa ukuta huo ni njia imara ya kujikinga na mashambulio ya kigaidi dhidi ya raia wake huku Bwana QOREI akikosoa hatua hiyo kuwa ya kibaguzi.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW