1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Ten Hag arefusha mkataba United

4 Julai 2024

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ameurefusha mkatabe wake mwaka wa 2026. Nafasi ya Mholanzi huyo ilikuwa katika hali ya sintofahamu katika msimu wa 2023-24 United ilipomaliza katika nafasi ya nane.

Erik ten Hag | Meneja | Manchester United
Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ameurefusha mkatabe wake mwaka wa 2026. Picha: Andrew Yates/Sportimage/Cal Sport Media/picture alliance/Newscom

Alibadilisha hayo kwa kuiongoza timu hiyo kubeba Kombe la FA kwa kuwabwaga Manchester City katika fainali ya Mei na sasa United wamempa mkataba mrefu.

Soma pia: Kikosi cha Manchester United kinaendelea kuandamwa na zimwi la kufanya vibaya kuanzia nyumbani hadi mechi za kimataifa

Ten Hag mwenye umri wa miaka 54, ameiambia tovuti ya klabu hiyo: "Nina furaha kufikia makubaliano na klabu ya kuendelea kuwa pamoja. Nikitizama miaka miwili iliyopita, tunaweza kujivunia makombe mawili tuliyobeba na mifano mingi ya hatua tulizopiga kutoka tangu nilipojiunga. Hata hivyo, lazima tuwe wazi kuwa bado kuna kazi ngumu ya kufanya mbele yetu ili kufikia viwango vinavyotarajiwa na Manchester United, kumaanisha kushindania mataji ya ligi kuu na ya Ulaya."

Tangazo kuhusu Ten Hag linajiri katika wiki ambayo Dan Ashworth hatimaye ameteuliwa kuwa mkurugenzi mpya wa spoti wa United baada ya miezi ya mazungumzo na waajiri wake wa zamani Newcastle.