Tergat kugombea urais wa Kamati ya Olimpiki Kenya
31 Machi 2017Matangazo
Kamati ya Olimpiki ya Kenya imekumbwa na matatizo tangu michezo ya Olimpiki iliyoandaliwa mjini Rio de Janeiro, Brazil.
Tergat alishinda mataji matano mfululizo ya dunia katika mbio za nyika kutoka mwaka wa 1995 hadi 2000 na medali mbili za fedha za Olimpiki katika mbio za mita 10,000. Anahudumu kwenye kamati kuu ya olimpiki Kenya.
NOCK itafanya uchaguzi mnamo Mei 5 baada ya kuidhinisha mabadiliko kwenye katiba yake wiki hii kufuatia ombi la Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.
Uongozi wa Keino uko chini ya uchunguzi baada ya maafisa wakuu wa NOCK kukamatwa kufuatia sakata la Olimpiki mjini Rio na kushitakiwa kwa wizi wa vifaa vya michezo na fedha.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman