1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Terzic ajiuziulu kama kocha wa Borussia Dortmund

13 Juni 2024

Edin Terzic amejiuzulu kama kocha wa Borussia Dortmund. Klabu hiyo ya Ujerumani ilifika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu imeyasema hayo katika taarifa ya kushangaza.

Kocha wa klabu ya Dortmund Edin Terzic
Kocha wa klabu ya Dortmund Edin TerzicPicha: Adrian Dennis/AFP/Getty Images

Dortmund imesema Terzic mwenye umri wa miaka 41 ameomba kusitisha mkataba wake maramoja na baada ya mazungumzo, klabu hiyo ikalikubali ombi lake.

Terzic alishinda Kombe la Shrikisho la Ujerumani - DFB Pokal akiwa na Dortmund mwaka wa 2021 kama kocha wa muda na kisha akawasaidia kumaliza katika nafasi ya pili katika Bundesliga mwaka wa 2023 na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwezi huu akiwa kocha wa kudumu.

Alipoteza fainali hiyo kwa Real Madrid iliyowafunga 2 - 0 katika dimba la Wembley mjini London, Uingereza.

Terzic, shabiki wa tangu utotoni wa Dortmund, amesema inauma sana kwake kutoa tangazo hilo kwa mashabiki wa Dortmund.

Ameongeza kuwa baada ya fainali ya Wembley, aliomba kufanya mkutano na viongozi waandamizi wa klabu kwa sababu baada ya miaka 10 katika timu hiyo ikiwemo mitano kwenye benchi la ufundi na miwili na nusu kama kocha mkuu, anahisi kuwa enzi mpya ya klabuinapaswa kuanza na kocha mpya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW