1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUturuki

Tetemeko jipya la ardhi lazikumba Uturuki na Syria

21 Februari 2023

Watu wasiopungua sita wamefariki dunia na mamia wamejeruhiwa kufuatia tetemeko jipya la ardhi ambalo limetikisa Uturuki na Syria usiku wa kuamkia leo Jumanne.

Türkei Hatay | Rettungsarbeiten nach dem letzten Erdbeben
Picha: Thaier Al-Sudani/REUTERS

Waziri wa mambo ya ndani nchini Uturuki Süleyman Soylu amesema hayo baada ya matetemeko mawili kutokea.

Kulingana na mamlaka ya Uturuki inayosimamia majanga (AFAD), tetemeko la kwanza lilikuwa na ukubwa wa 6.4 kwenye vipimo vya ritcha na la pili lilikuwa na ukubwa wa 5.8 kwenye vipimo vya ritcha, na lilitokea dakika tatu baadaye,

Shirika la Kandili, linalofuatia matetemeko ya ardhi nchini Uturuki, limesema kitovu cha tetemeko la hivi karibuni ni wilaya ya Samandag  Uturuki.

Shirikahilo, limeongeza kuwa tetemeko hilo limehisiwa hadi Jordan, Israel, Lebanon na Misri.

Matetemeko hayo, yamejiri wiki mbili baada ya matetemeko mabaya ya ardhi yaliyotokea Uturuki na Syria na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 47,000.