1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Tetemeko la Ardhi Bangladesh lasababisha mauaji ya watu 4

21 Novemba 2025

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.5 katika kipimo cha Richter, limepiga Bagladesh na sehemu kadhaa za India leo Ijumaa na kusababisha vifo vya watu wanne huku wengine wengi wakijeruhiwa.

Bangladesch Dhaka 2025 | Tetemeko la ardhi
Tetemeko la Ardhi Bangladesh lasababisha mauaji ya watu 4 Picha: MD Nahid Anjuman/DW

Kwa mujibu wa Shirika la kuchunguza matetemeko ya ardhi la Marekanila USGS, tetemeko hilo lilipiga maeneo hayo na athari zake zilishuhudiwa katika eneo la Ghorashal huko Bangladesh.

Tetemeko hilo lililodumu kwa sekunde kadhaa liliyumbisha majengo kadhaa na kusababisha  hofu miongoni mwa raia waliokimbilia barabarani.

Mashirika ya huduma ya zimamoto na mashirika ya dharura ya ulinzi wa raia yaliripoti kuwepo kwa nyufa kadhaa katika majengo mengi mjini Dhaka.

Mtoto wa miezi 10 ni miongoni mwa waliouwawa wakati kuta ya nyumba yao ilipomuangukia.