JangaChina
Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.1 lapiga eneo la Xinjiang
23 Januari 2024Matangazo
Kulingana na idara ya hali ya hewa ya China, tetemeko hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo na limepiga karibu na mkoa wa Xinjiang kaskazini magharibi mwa China.
Shirika la habari la serikali Xinhua limeripoti kuwa, kampuni ya reli imesitisha mara moja safari zake huku treni 27 zikiathirika na tetemeko hilo la ardhi.
Mamlaka ya kukabiliana na majanga imesema tayari imetuma timu ya uokoaji katika eneo la mkasa.
Katika muda wa saa 24 zilizopita, mkoa wa Xinjiang na viunga vyake umekumbwa na matetemeko kadhaa ya ardhi.
Nchi jirani ya Kazakhstan, idara zinazohusika na kukabiliana na majanga zimeripoti tetetemo la ardhi la ukubwa wa 6.7.
Mitetemeko mengine ya ardhi imeripotiwa pia nchini Uzbekistan.