1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUturuki

Tetemeko la ardhi lenye lapiga mashariki mwa Uturuki

16 Oktoba 2024

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 kwenye kipimo cha Richter limepiga katika jimbo la Malatya mashariki mwa Uturuki. Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 lapiga mashariki mwa Uturuki
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 lapiga mashariki mwa UturukiPicha: Tsubasa NARISHIMA/AP/picture alliance

Tetemeko hilo limeripotiwa pia katika mikoa jirani ya Elâzig na Diyarbakir. Meya wa mji mkuu wa mkoa wa Malatya, Sami Er amesema hakukuwa na taarifa zozote za majeruhi au uharibifu, huku mamlaka ikitoa wito kwa wakaazi kusalia nje kwa sasa.

Oktoba 6 mwaka jana, watu 1,000 walikufa katika jimbo la Malatya kulipotokea matetemeko makubwa ya ardhi yaliyopiga kusini-mashariki mwa Uturuki na katika nchi jirani ya Syria na kusabisha vifo vya watu zaidi ya 50,000.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW