1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Tetemeko la ukubwa wa 6.3 lapiga Magharibi mwa Afganistan

Hawa Bihoga
7 Oktoba 2023

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 katika kipimo cha Richter, limetokea Magharibi mwa Afghanistan leo Jumamosi. Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani, limesema tetemeko hilo liliambatana na mengine matatu.

Marokko | Aufräumarbeiten und Hilfe nach Erdbeben
Picha: Ammar Awad /REUTERS

Hadi sasa hakuna taarifa za vifo wala uharibifu wa majengo, lakini taarifa ya Shirika la Utafiti wa jiolojia Marekani imeonya kwamba huenda kukawa na maafa. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika kiwango hicho cha tahadhari kunahitajika mwitikio wa ngazi ya kikanda au kitaifa.

Soma pia:Waliofariki tetemeko la ardhi nchini Morocco yafika 2,901

Itakumbukwa kuwa, mwezi Juni mwaka uliopitazaidi ya watu 1,000 walikufana maelfu waliachwa bila makaazi baada ya tetemeko la ukubwa wa 5.9 ambalo ni baya zaidi nchini humo kwa kipindi cha robo karne kupiga jimbo masikini la Paktika. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW