1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetesi za uhamisho wa wachezaji barani Ulaya zapamba moto

16 Juni 2023

Vilabu barani Ulaya vipo kwenye heka heka ya kuanza kuimarisha vikosi vyao kuelekea msimu ujao. Kila timu inaangalia namna gani itaweza kujiandaa na mashindano mbalimbali yanayotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.

UEFA Champions League Villarreal v Liverpool
Giovani Lo Celso, Mchezaji wa Tottenham Hotspurs.Picha: Eric Alonso/Getty Images

Lo Celso kwenye rada ya Barcelona.

Barcelona wamemuweka kiungo wa kati wa Tottenham Giovani Lo Celso kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa katika majira ya kiangazi.

Bosi wa Barcelona Xavi anavutiwa sana na mchezaji huyo na amemweka miongoni mwa viungo vyake vya kutafuta sokoni.

Barca wako tayari kujadili dili la Lo Celso na Spurs iwapo watakubaliana huenda wakamrejesha Clement Lenglet ambaye alikuwa Spurs 

Lenglet amerejea Barca kufuatia mkopo wa msimu mzima na anasalia kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Spurs.

Barca wanatazamia kusajili angalau kiungo mmoja mpya, huku pia nyota wa Manchester City Ilkay Gundogan akiwa kwenye rada ya kutimkia Barcelona, Gundogan atakuwa mchezaji huru Julai 1 .

Bernardo Silva na Manchester City bado kizungumkuti.

Man City haitaweka kiwingu kwa Bernardo Silva kama anataka kuondoka katika klabu hiyo.

Bernardo Silva, mchezaji wa Manchester City akishangilia goli katika mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Mancester City na Real Madrid.Picha: Clive Brunskill/Getty Images

Klabu ya Paris Saint-German ya nchini Ufaransa ina nia ya kumsajili mchezaji huyo huku pia Barecelona wakitajwa kuingia katika rada hizo za mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno.

Msimu uliomazika Manchester City wamekuwa na wakati mzuri na timu hiyo bado inayo nia ya kutaka kumbakisha nyota huyo kwa muda mrefu, akiwa na timu yake msimu huu wameshinda Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Premia na Kombe la FA.

Hata hivyo, Silva anatajwa kuwa anafikiria  kuondoka City msimu uliopita wa joto, jambo ambalo halikutimia.

Dili la Declan Rice lawakosesha amani washika mitutu wa London.
 

Nahodha wa West Ham United Declan Rice akiwa katika moja ya ligi kuu ya Premia mchezo dhidi ya Leicester City.Picha: MI News/NurPhoto/picture alliance

Klabu ya soka ya Arsenal imegonga mwamba kwa wagonga nyundo wa London West Ham baada ya ofa yao ya awali ya pauni milioni 80 kukataliwa, Nahodha wa West Ham na nyota wa kimataifa wa England, Declan Rice anawindwa na klabu za Arsenal, Manchester City, Bayern Munich na Manchester United.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW