TEXAS: Mripuko wauwa watu 14 Marekani
24 Machi 2005Matangazo
Idadi ya waliofariki inaongezeka kufuatia Mripuko mkubwa katika kiwanda cha kusafishia mafuta nchini Marekani, ambapo tayari takriban watu 14 wameuwa na kuwajeruhi zaidi ya wengine 70.
Mripuko huo uliosababisha hasara kubwa katika mtambo mkubwa wa kampuni ya mafuta ya BP ,ulitikisa majengo yaliyoko karibu.
Msemaji wa Bp hakuweza kudhibitisha chanzo cha mripuko huo lakini maafisa wa serikali wamesema hawafikirii kuhusika kwa magaidi. Wahudumu wa matukio ya dharura wamewaonya wanaoishi karibu na eneo hilo kubakia majumbani mwao.
Kiwanda hicho kinatoa asilimia 30 ya mafuta ya vituo vya Bp vilivyo Amerika ya Kaskazini na asilimia 3 ya kiwango cha mafuta yanayosambazwa nchini Marekani.