1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Thailand yafikiria kusitisha kuiuzia mafuta Cambodia

14 Desemba 2025

Jeshi la Thailand limebainisha kuwa linafikiria kuzuia mauzo ya mafuta kwa Cambodia wakati mapigano kati ya nchi hizo mbili yakiendelea kusambaa katika maeneo ya Pwani katika mpaka unaozozaniwa.

Thailand na Cambodia zimekuwa na mzozo wa mara kwa mara unaohjusu mpaka wao wa zaidi ya kilomita 800
Mwanajeshi wa Cambodia akiwa kwenye gari la kijeshi lenye uwezo wa kuyatua makomboraPicha: AFP/Getty Images

Msaidizi wa msemaji wa jeshi la wanamaji la Thailand Kepteni Nara Khunkothom, ameeleza kuwa Makamanda wa jeshi la nchi hiyo wamelitaka pia jeshi la wanamaji kuwa makini dhidi ya meli zinazobeba bidhaa muhimu za kimkakati.

Maeneo ya Bahari karibu na bandari za Cambodia kutangazwa kuwa ya hatari

Wamejadili pia juu ya uhitaji wa kuyatangaza maeneo ya Bahari karibu na bandari za Cambodia kuwa "ya hatari kubwa”. Thailand inafikiria kuchukua hatua hiyo saa kadhaa baada ya kutangaza amri ya kutokutoka nje katika mkoa wake wa kusini mashariki wa Trat wakati mzozo kati ya nchi hizo na Asia ukipamba moto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW