Thamani ya sarafu ya Euro imevunja rekodi
27 Februari 2008Matangazo
NEW YORK:
Thamani ya sarafu ya Euro imevuka Dola 1,50 katika masoko ya sarafu za kigeni na hivyo imevunja rekodi yake huku kukiwepo hofu kwamba uchumi wa Marekani unazidi kuzorota.Lakini Rais wa Marekani George W.Bush amekanusha ripoti zinazosema kuwa uchumi wa nchi hiyo upo katika hatari ya kudhoofika zaidi.Bush amesema, uchumi unakwenda pole pole na wala haukudorora.