1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

The Hague. Afisa wa zamani wa polisi nchini Macedonia asema hana hatia katika shtaka la uhalifu wa kivita katika mahakama ya The Hague.

18 Aprili 2005

Afisa wa zamani wa polisi wa Macedonia amedai kuwa hana hatia kutokana na shtaka la uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa mjini The Hague. Johan Tarculovski anashitakiwa kwa mauaji, uharibifu wa mali na ukatili kufuatia shambulio lililofanywa na jeshi la polisi katika kijiji karibu na mji mkuu Skopje mwaka 2001. Afisa huyo mwenye umri wa miaka 30 alishtakiwa pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Macedonia Ljube Boskovski ambaye hapo kabla alisema hana hatia kutokana na mashtaka kama hayo.

Macedonia ilipigana vita vya miezi sita na wanamgambo katika mwaka 2001. Serikali ya kizalendo ya nchi hiyo ilipigana kuzima dhidi ya uasi kutoka kwa wanamgambo wenye asili ya Albania ambao ni wachache nchini humo.

Majeshi ya NATO na umoja wa Ulaya yalisitisha mapigano hayo, na kupelekea kupatikana kwa makubaliano ya amani ya Ohrid na kupatiwa kwa madaraka ya zaidi kwa raia hao wenye asili ya Albania.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW