1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Uchunguzi juu ya uhalifu wa vita Darfur wapiga hatua

30 Juni 2005

Mshtaki mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague amesema anapiga hatua katika uchunguzi wake juu ya mauaji yaliyofayika nchini Sudan katika jimbo la Darfur.

Luis Moreno Ocampo ameliambia baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba serikali ya Khartoum inastahili kushirikiana na mahakama ya The Hague.

Kesi juu ya mauaji ya Darfur ndio ya kwanza kuwahi kufikishwa mbele ya mahakama hiyo na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,lakini serikali ya Khartoum imesema haitawahukumu watuhumiwa watakaorejeshwa nchini humo na badala yake imesema itawafungulia mashataka washukiwa 160.

Watu laki 1 na elfu 80 wameuwawa katika eneo la Darfur kufuatia mapigano,njaa na maradhi huku wengine milioni mbili wakiachwa bila makao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW