1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THESSALONIKII:Polisi wapambana na waafrika wanaopinga kifo cha mwenzao nchini Ugiriki

21 Agosti 2007

Polisi wa Ugiriki wamepambana na wahamiaji wa kiafrika katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Thessaloniki waliyokuwa wakipinga mauaji ya mhamiaji wa kinigeria mwisho mwa wiki.

Kijana huyo wa Kinigeria alifariki baada ya kuruka kutoka kwenye jengo moja alikokuwa akiuza dvd zilizodurufiwa, baada ya kuhofu kuwa polisi walikuwa wakitaka kumkamata.

Hata hivyo polisi katika mji huo wamesema kuwa kulikuwa hakuna afisa yoyote wa polisi aliyetaka kumkamata.

Waandamanaji hao wakiwa na picha za mtu huyo walipambana na polisi ambao walilazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW