1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thiago aurefusha mkataba wake na Bayern

28 Agosti 2015

Kiungo wa Bayern Munich Thiago Alcantara amekubali kuurefusha mkataba wake na klabu hiyo kwa miaka miwili hadi 2019. Mhispania huyo analenga kujaza pengp la Bastian Schweinsteiger

Fußball Champions League Viertelfinale Rückspiel FC Bayern München - FC Porto
Picha: picture-alliance/dpa/J. Gebert

Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la “Bild” Thiago sasa ataweka mfukoni kiasi cha hadi euro milioni tisa kwa mwaka katika marupurupu.

Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenige amesema wana furaha kwa Thiago amekubali kubakia katika klabu hiyo.

Mhispania huyo hajawa na mwanzo mzuri katika klabu yake hiyo tangu alipojiunga mwaka wa 2013 kutoka Barcelona kutokana na matatizo ya goti. Alikuwa mkekani kwa karibu mwaka mmoja. Alirejea Aprili 2015 na kufikia sasa amecheza michuano 25 ya Bundesliga huku akifunga magoli manne na kusaidia katika mengine manne.

Leverkusen wampoteza Son Heung-min

Bayer Leverkusen tayari wamempoteza mshambuliaji wao Mkorea Kusini Son Heung-Min. Son amejiunga na klabu ya ligi ya Premier ya England, Tottenham Hotpur. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amesaini mkataba wa kiasi cha pauni milioni 22 na Tottenham. Kocha Roger Schmidt anasema wameumizwa na kuondoka kwa mshambuliaji huyo. “Nadhani ni habari za huzuni. Bila shaka naamini kuwa mchezaji hufikiria kuhusu taaluma yake na kisha hutaka kuhamia klabu nyingine katika wakati muafaka. Hiyo ni halali na sawa kabisa. Hivyo ndivyo biashara ya kandanda ilivyo. Lakini bila shaka alikuwa ameingiana nasi na kuiozea kabisa timu, hata kihisia, hivyo ningetamani kuwa hali hii ingekuwa tofauti“.

Mwandishi: Bruce Amani/DW
Mhariri: