Thuluthi mbili ya majengo ya Gaza yameharibiwa - UM
30 Septemba 2024Matangazo
Kulingana na picha zilizokusanywa na kituo cha satelaiti cha Umoja wa Mataifa, UNOSAT, tangu mwaka uliopita hali imezidi kuwa mbaya.
Kwa mujibu wa taarifa mpya ya kituo hicho, majengo zaidi ya 50,000 yameteketezwa na mengine 18,913 yameharibiwa vibaya.
Soma zaidi: Watu 15 wauwawa katika shambulizi la Israel katika shule ya Gaza
UNOSAT pamoja na Shirika la Chakula la Umoja Mataifa (FAO) zimesema asilimia 68 ya mazao kwenye mashamba yameathirika.
Asasi hiyo ya Umoja wa Mataifa imekuwa inafanya kazi kwa lengo la kutoa taarifa sahihi jinsi majengo na miundombinu ilivyoathirika kutokana na vita kwenye Ukanda wa Gaza.