TI yaonya kuhusu ufisadi katika kandanda
20 Novemba 2015Mkurugenzi mkuu wa TI Cobus de Swardt amesema katika taarifa kuwa hatari ya ufisadi katika mashirikisho mengi sana ya kandanda ulimwenguni ni kubwa.
Uchunguzi huo unafuatia upelelezi wa uhalifu ulioanzishwa na waendesha mashtaka nchini Marekani na Uswisi dhidi ya FIFA na maafisa wakuu wa kandanda. TI imependekeza kuwa uchunguzi wa mpana wa fedha unapaswa kuwa sehemu muhimu ya kubadilisha utamaduni wa FIFA na wanachama wake.
Ni wanachama 14 pekee – wakiwemo England, Italia, na mashirikisho yote matatu ya Scandinavia – yanayochapisha habari chache inayopendekezwa na TI. Tatu tu kati ya 14 ni wa nchi ya Ulaya: Canada, Japan na New Zealand.
Zaidi ya moja kati ya tano ya mashirikisho 209 ya kitaifa ya kandanda hayana tovuti ya kueleza kazi zao, na 178 hayachapishi ripoti ya kila mwaka ya shughuli zake
Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/AP/Reuters
Mhariri:Yusuf Saumu