TIBU-zahanati ya kuhamishwa nchini Kenya
28 Mei 2020
Nathalie Maikere ameketi katika meza ya chakula, umbali si mrefu watoto wake wawili wanaonekana wakicheza michezo ya vidio kwenye kompyuta yao huku daktari akimpima Maikere halijoto ya mwili wake, pigo la mwoyo na shinikizo la damu.
Maikere ni moja miongoni mwa zaidi ya wakaazi 600 wa mjini Nairobi wa Kenya wanaopokea huduma za matibabu na afya kupitia mpango, TIBU- zahanati ya kuhamishwa ambayo hutoa matibabu kwa wagonjwa wakiwa nyumbani kwao.
Mpango huo uliozinduliwa mnamo Machi, ni baadhi ya mipango inayonuia kuleta huduma za afya kwa wagonjwa hata wakiwa kwao nyumbani.
Uzinduzi wa wake ulisadifiana na wakati janga la virusi vya Corona ambao umelazimisha idadi kubwa ya watu kusalia ndani.
''Watu wengi hufikiria tu kwenda zahanati au hospitalini pindi wanapougua, hawatambuwi kuwa mara nyingi huhitaji hata kwenda hospitalini au kufahamu kuwa hata zahanati yenyewe inaweza kukufikia ukiwa nyumbani kwako.'' Amesema Jason Carmichael, mkrugenzi mkuu wa TIBU, zahanati hiyo pia hufanya vipimo vya ugonjwa wa COVID-19 ameongeza.
Kulingana Carmichael mteja au mgonjwa hutumia App ya simu yake ya mkononi kuomba matibabu na kisha kuunganishwa na daktari aliye karibu naye kupitia mtandao, daktari humpigia simu mgonjwa na baadaye kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwake.
Makampuni ya Marekani ya kutoa huduma ya afya ikiwemo Heal lenye makao yake Los Angels na Page kutoka New York yamekuwa yakiendelea kutoa huduma hizo nchini Kenya, hatahivyo kwa bei ghali.
TIBU humlipisha mgonjwa shillingi elfu moja ya Kenya chini ya dola 10 za Marekani kwa huduma ya kuomba ukaguzi wa daktari, hii inamaanisha kuwa huenda zahanati hiyo inalenga kuhudumia watu wa tabaka la wastani.
Wanzilishi wa TIBU wanasema katika kipindi hiki cha janga la COVID-19, watu wengi wameomba huduma ya afya kutoka zahanati hiyo kutokana na kile walichoeleza kuwa wengi wao kuogopa kwenda hospitalini kwa hofu ya kuambukizwa na virusi hatari vya Corona.
Chanzo: RTRE