1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tim Walz asifu miaka minne ya uongozi thabiti wa Biden

22 Agosti 2024

Gavana wa Minnesota Tim Walz amekubali rasmi uteuzi wa chama cha Democrat kuwa mgombea mwenza wa Kamala Harris. Katika hotuba yake amesema kuteuliwa kuwa mgombea mwenza ni “heshima kwake.”

Marekani | Siasa | Mgombea Mwenza wa urais wa Demokratiki Tim Walz.
Mgombea Mwenza wa urais Marekani kupitia tiketi ya chama cha Demokratiki Tim Walz.Picha: Brendan McDermid/REUTERS

Gavana huyo mwenye umri wa miaka 60 pia amewashukuru wajumbe na wafuasi wa chama hicho kwa kuweka imani kwake.

"Kwanza natoa shukrani kwa Makamu wa Rais Kamala Harris. Asante kwa kuweka imani yako kwangu na kwa kunialika kuwa sehemu ya kampeni hii bomba. Asante pia kwa Rais Joe Biden kwa miaka minne ya uongozi dhabiti wa kihistoria."

Soma pia:Walz akubali rasmi kuwa mgombea mwenza wa Kamala Harris

Ameeleza baadhi ya sera watazozitekeleza iwapo watachaguliwa, ni pamoja na kupunguza ushuru kwa familia za tabaka la kati, kupunguza bei za dawa na kulinda haki ya uhuru wa mtu binafsi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW