1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu kujikatia tiketi ya fainali Champions League

2 Mei 2022

Mashindano ya Ligi ya Mabingwa UIaya yanaelekea fainali yake ya tatu katika misimu minne itakayozikutanisha timu mbili za England isipokuwa kama wapinzani wao wa Uhispania wataweza kuyapindua matokeo ya mkondo wa kwanza

Manchester City vs Real Madrid - UEFA Champions League
Picha: David Ramos/Getty Images

Mashindano ya Ligi ya Mabingwa UIaya yanaelekea katika fainali yake ya tatu katika misimu minne itakayozikutanisha timu mbili za England isipokuwa kama wapinzani wao wa Uhispania wataweza kuyapindua matokeo ya mkondo wa kwanza.

Villarreal ilipitiliza matarajio yao na kufika nne bora baada ya kuwaduwaza mabingwa wa zamani Juventus na Bayern Munich na sasa itakutana kesho Jumanne na Liverpool iliyoshinda 2-0 katika mkondo wa kwanza Anfield.

Liverpool wanawinda mataji manne msimu huu, ya Champions League, ligi kuu England, Kombe la FA na Kombe la Ligi.

Baada ya mechi ya kuburudisha pakubwa na kushuhudia mabao saba, ni mechi mkondo wa pili inayosubiriwa kwa hamu na ghamu ya mabingwa mara 13 wa Ulaya Real Madrid dhidi ya mashine ya ushambuliaji ya Pep Guardiola Manchester City. City ilishinda mechi ya nyumbani 4-3. Na Madrid ambao tayari wameshinda ubingwa wa 35 wa La Liga waliwapumzisha baadhi ya wachezaji nyota katika mechi yao ya mwishoni mwa wiki dhidi ya Espanyol. City ipo katikati ya mapambano ya ubingwa wa ligi dhidi ya Liverpool na pia iliwapumzisha wachezaji wake nyota.

reuters

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW