1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Al Ahly ya Misri yashinda ligi ya mabingwa barani Afrika

12 Juni 2023

Timu ya Al Ahly ya Misri imeibuka kidedea kwa bao la kusawazisha dakika za lala salama na kupata sare ya 1-1 dhidi ya watetezi Wydad Casablanca ya Morocco na kutwaa ligi ya mabingwa barani Afrika

Ägypten | CAF Champions League 2022/23 | Finale – Al Ahly gegen Wydad
Picha: Weam Mostafa/Sports Inc/empics/picture alliance

Beki Mohamed Abdelmoneim aliunganisha mpira safi wa kona kutoka kwa Ali Maaloul zikiwa zimesalia dakika 13, mpira ukiwapita walinzi na kuingia kwenye kona ya wavu na kuipa klabu hiyo ya Cairo taji la 11 lililoongeza rekodi kubwa ya mataji.

Wydad walikuwa mbioni kushinda kwa sheria ya bao la ugenini

Baada ya kupoteza 2-1 katika mji mkuu wa Misri katika mchezo wa mkondo wa kwanza Jumapili iliyopita, Wydad walikuwa kwenye mbio za kushinda kwa sheria ya bao la ugenini baada ya beki wa pembeni Yahya Attiat Allah kufunga kunako dakika ya 27 mbele ya umati mkubwa wa takribani watu 50,000 kwenye Uwanja wa Mohamed V wa Casabalanca.