1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu ya Argentina yarejea nyumbani kutoka Qatar

20 Desemba 2022

Timu ya Argentina ambao ni mabingwa wapya wa Kombe la Dunia, wamewasili leo asubuhi nyumbani wakitokea Qatar na kulakiwa na maelfu ya mashabiki.

Argentinien Weltmeister erreichen Buenos Aires
Picha: Agustin Marcarian/REUTERS

Sherehe kubwa zimeandaliwa kufanyika baadae leo, ikiwemo gwaride kubwa kwa ajili ya Lionel Messi na wachezaji wenzake. Messi aliyekuwa amelibeba kombe mikononi mwake, alikuwa wa kwanza kushuka kwenye ndege pamoja na kocha wa Argentina, Lionel Scaloni.

Rais wa Argentina, Alberto Fernández ameitangaza siku ya leo kuwa ya mapumziko ya kitaifa ili kumuwezesha kila mmoja kulisherehekea kombe hilo.

soma zaidi:Maoni: Messi ndie bora zaidi kombe la Dunia 2022

Shirikisho la Kandanda la Argentina limesema kuwa timu hiyo itasherehekea ushindi huo pamoja na mashabiki katika eneo maarufu la Plaza de la Republic kwenye mji mkuu, Buenos Aires, ambako kuna mnara wa Obelisk.

Argentina iliibuka mshindi baada ya kuifunga Ufaransa kwa mikwaju ya penalti siku ya Jumapili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW