1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Timu ya kampeni ya Kamala Harris yakusanya dola milioni 540

26 Agosti 2024

Timu ya kampeni ya makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris imekusanya dola milioni 540 kwa ajili ya kupiga jeki azma yake ya kuwania urais atakapopambana na mgombea wa Republican, rais wa zamani Donald Trump.

USA Chicago | Präsidentschaftskandidatin Kamala Harris
Makamu wa rais wa Marekani Kamala HarrisPicha: Kevin Lamarque/REUTERS

Kiongozi wa timu hiyo ya kampeni Jen O'Malley Dillon amesema kuwa, kabla ya Kamala Harris kutoa hotuba ya kukubali rasmi uteuzi wa chama cha Democratic kuwa mgombea urais siku ya Alhamisi, tayari walikuwa wamekusanya zaidi ya dola milioni 500.

O'Malley ameeleza kuwa, karibu theluthi moja ya michango wiki iliyopita ilitoka kwa wachangiaji waliotoa kwa mara ya kwanza.

Soma pia: Kamala kutoa hotuba ya aina yake kukubali uteuzi 

Takriban asilimia 20 ya wachangiaji hao wa mara ya kwanza walikuwa wapiga kura vijana huku theluthi mbili wakiwa wanawake; makundi ambayo yanachukuliwa kuwa muhimu kwa Harris kupata ushindi katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Kampeni hiyo imeshuhudia ongezeko la michango wakati wa kongamano la kitaifa la chama cha Democratic lililofanyika mjini Chicago ambapo Kamala Harris na mgombea mwenza wake, gavana wa Minnesota Tim Walz walikubali rasmi uteuzi wao.