1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu ya kandanda ya Kenya kucheza na Burundi

12 Februari 2023

Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) limetangaza kuwa timu ya Kenya itacheza na Burundi katika mechi mbili za kirafiki mwezi Machi.

FIFA Logo
Picha: APTN

Hiyo itakuwa mechi ya kwanza ya kimataifa ya kandanda tangu marufuku ya mwaka mmoja ya Shirikisho la soka la kimataifa FIFA kuondolewa mwezi Novemba mwaka jana.

Mnamo Februari 2022, shirikisho la soka duniani lilichukua hatua ya kulisimamisha shirikisho la FKF, likitaja kuingiliwa na serikali baada ya mamlaka kulifunga shirika hilo mwaka 2021 kwa madai ya ufisadi.

Mkuu wa sasa wa Shirikisho la soka la Kenya  Barry Otieno amesema kurejea kwa timu ya taifa katika mechi mbili za kirafiki zilizopangwa Machi 25 na 28 jijini Nairobi ni maendeleo chanya kwa nchi hiyo, na ni hatua ya kwanza katika kuijenga upya timu na kuwaweka tayari kwa soka la kimataifa lenye ushindani. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW