1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu ya soka ya wanawake ya Ujerumani yabeba medali ya shaba

9 Agosti 2024

Ujerumani imepata medali ya shaba katika mashindano ya soka ya Olimpiki ya wanawake baada ya kuibwaga Uhispania bao 1-0 kufuatia mkwaju wa penalti wa Giulia Gwinn.

Paris 2024 -Ujerumani
Nyota wa Ujerumani Giulia Gwinn ameibuka kidedea kwa kuidaka penalti ya nyota wa Uhispani Alexia Putellas katika dakika za mwisho wa mchezo Picha: Marcus Brandt/dpa/picture alliance

Ujerumani imepata medali ya shaba katika mashindano ya soka ya Olimpiki ya wanawake baada ya kuibwaga Uhispania bao 1-0 kufuatia mkwaju wa penalti wa Giulia Gwinn baada ya mabingwa hao wa dunia kukosa penalti ndani ya muda wa ziada kwenye Uwanja wa Lyon.

Ujerumani, ambao walishindwa na Marekani katika mchezo wa nusu fainali, walipata bao la kuongoza katika dakika ya 65 baada ya Gwinn kupata penati hiyo na kufunga baada ya kuchezewa vibaya na kipa wa Uhispania Cata Coll.

Alexia Putellas wa Uhispania alipoteza nafasi ya kuipeleka mechi katika muda wa ziada baada ya penalti yake kuokolewa na kipa Ann-Katrin Berger katika sekunde za mwisho za mechi.