Timu ya wasichana ya Ujerumani mabingwa wa dunia.
1 Oktoba 2007Paul Tergat wa Kenya, asema anarudi uwanjani kurejesha rekodi yake ya dunia iliovunjwa jana mjini Berlin na rafiki na hasimu yake Muethiopia
Haile Gebreselassie:
Katika Bundesliga,Bayern Munich imefungua mwanya wa pointi 4 kileleni baada ya kuizaba jumamosi bayer Leverkusen bao 1:0.
Ujerumani ni mabingwa tena wa kombe la dunia la FIFA.Timu ya wasichana was Ujerumani kwa mara ya pili imeibuka mabingwa baada ya jana kuizaba ile ya Brazil mabao 2:0.Sio tu Ujerumani imetwaa ubingwa bali katika mashindano haya haikufungwa hata bao 1 na hii ni rekodi.
Mshambulizi na staid wao Birgit Prinz aliufumania kwanza malngo wa Brazil mnamo dakika ya 52 ya mchezo na kipa wa Ujerumani, Nadine Angerer alizima mkwaju wa penalty wa stadi wa Brazil Marta.Akielezea jinsi alivyounyakua ,Nadie amesema:
“Katika mkwajuw a penalty,nilikwishamuangalia Marta alivyopiga penalty dhidi ya Australia.Alichagua pembe ya kushoto na mara hii nikadhani atapiga ya kulia na nikaenda upande huo na nikaokoa.”Kipa Nadine.
Huku Brazil ikipigana kufa kupona kusawazisha bao la Birgit,Simone Laudehr,akaupiga msumari wa pili na wa mwisho katika jeneza la Brazil katika kombe hili la dunia kwa bao lake maridadi mnamo dakika ya 86 ya mchezo.
Kwa kweli Brazil ndio iliotamba zaidi,alkini ni Ujerumani iliotia mabao.Ujerumani sasa ikirudi na kombe hadi Berlin, inapanga kuania kuandaa kombe lijalo 2001 na kanzela Angela Merkel wa Ujerumani hakukawia kuwapongeza wasichana wa Ujerumani kwa ushindi wao dhidi ya Brazil:
“Pongezi nyingi kwa kutwaa ubingwa na sasa tutatia hima kubwa kuona kombe lijalo la dunia la wanawake litachezwa Ujerumani.”-alisema Kanzela Angela Merkel.
Katika MPAMBANO WA KUANIA NAFASI YA 3 Marekani iliizaba Norway mabao 4:1.
Ama katika Bundesliga-Bayern Munich imeanza msimu kwa kishindo.Jumamosi iliizaba Bayer Leverkusen bao 1:0 na kufungua mwanya wa pointi 4 kileleni.Ilikua tena Luca Toni alielifumania lango la Leverkusen .Bayern munich haikushindwa tangu kuanza msimu huu na imekusanya pointi 20 kutoka mechi 8 na Leverkusen kwa pigo la jumamosiu imeteleza kutoka nafasi ya pili hadi ya 4.
Katika Premier League-Ligi ya Uingereza,tangu Manchester United hata Arsenal zimejipatia ushundi wao 5 na zinaongoza kileleni wakati Chelsea ilishindwa tena kutamba na kumudu sare 0:0 nyumbani na Fulham.Bao la Robin van Persie liliipatia Arsenal ushindi huo.Manchester iliilaza Birmingham City kwa bao 1-0.
Tugeukie sasa medani ya riadha:
Muethiopia Haile Gebreselassie wa Ethiopia jana aliivunja rekodi ya dunia yam bio za marathon ya mkenya paul Tergat.
Gebre alikimbia muda wa masaa 2: dakika 4 nasek 26 mjini Berlin na kuipangusha rekodi ya Paul tergat alioiweka katika jiji hilo hilo 2003.
Gebrselassie ni bingwa mara 2 wa olimpik na mara 4 wa dunia katika mita 10.000.tangu changamoto yake katika michezo ya olimpik ya Sydney, 2000,uhasama kati yake na mkenya Paul Tergat ulipambamoto.
Paul Tergat,ameeleza jana kwamba hapangi kustaafu na anarudi uwanjani kusaka rekodi nyengine.
Wanariadha 24 wa Tanzania wakijandaa kwa michezo ijayo ya Olimpik ya Beijing, wameffunga safari kwenda China.