1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu zilizoingia nusu fainali kombe la dunia zakamilika

Sekione Kitojo
8 Julai 2018

Karibu  katika  awamu ya fainali ya timu  nne zitakazokuwamo  katika  nusu  fainali  ya kombe  la dunia, huenda ikiwa ni timu  ambazo  hazikutarajiwa  katiba  katika  mashindano haya  ya  21  ya  dunia.

Fußball WM 2018 Schweden - England
Picha: Reuters/M. Rossi

Chakula maarufu nchini  Uingereza  cha  samaki na Chips dhidi  ya chakula maarufu  cha  Croatia cha Samaki Risotto. Kinywaji  cha  Ufaransa cha Vin et fromage dhidi  ya bia  ya Ubelgiji.

Wenyeji Urusi waliondoka  uwanjani  usiku wa  Jumamosi  wakidondokwa machozi , baada ya  kutoka  sare  dhidi  ya  Croatia  kwa  mabao 2-2 na mchezo  huo  kuingia  katika  dakika za  nyongeza na  hatimaye  kushindwa  kwa mikwaju  ya  penalti.

Timu mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia Urusi imetolewa katika mashindano katika robo fainaliPicha: Reuters/M. Shemetov

Wajurumani  ambao  huwa  makini  sana  waliondolewa  mapema, pamoja  na  kikosi  cha Samba  cha  Brazil  pamoja  na  tiki taka ya  Uhispania.

Argentina  ya Lionel Messi   na  Cristiano  wa  Ureno  hawakuweza  kuvuka  kiunzi cha  timu 16  bora. Azzurri  ya  Italia  haipata  hata  fursa  ya  kualikwa   hata  kufikia  katika  awamu  hii ya  fainali.

Cristiano Ronaldo (kushoto)akimsaidia Cavani kutoka nje wakati wa pambano baina ya Ureno na UruguayPicha: Reuters/J. Silva

"Yeyote  ambaye alipigiwa  upatu  kutoroka  na  taji  hili, timu  vigogo , ziko  nyumbani," kocha wa  Croatia Zlatko Dalic  alisema  kupitia  mkalimani. Wale  waliofanya  kazi kwa  bidii , ambao  wanacheza  kama  timu, wako  pamoja  na  ambao  wamejiandaa  vizuri , bado wako  hapa  Urusi, na  hii  ndio hali  ya  timu  nne zilizobakia  katika  kinyang'anyiro  hiki."

Kinyang'anyiro  cha  kwanza  kitakuwa  kati  ya  Les Bleus dhidi  ya  De Rode Duivels siku  ya Jumanne  usiku  mjini  St. Petersburg,  pambano  la  majirani  kutoka  bara  la  Ulaya.

Pambano  kati  ya  Simba  watatu dhidi  ya  Vatreni  litafuatia  usiku wa siku  ya  Jumatano mjini  Moscow.  Je kandanda  linarejea  nyumbani  ama  taji  litakwenda  sehemu  nyingine mpya ?

"tumo  katika  nusu  fainali  ya  kombe  la  dunia. Iwapo tumo katika  timu  nne bora  duniani bado  ni  kitu  ambacho tunapaswa  kuthibitisha," Meneja  wa  England Gareth Southgate alisema. "Itakuwa  ishara  kwa  vilabu  vyote  kwamba, iwapo  ni  England  ama  kwingineko, kwamba  wachezaji  wa  Uingereza  wanaweza  kucheza  soka, kwamba  tuna  wachezaji ambao wana ustadi  mkubwa.

Kocha wa Uingereza Gareth SouthgatePicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Timu bora za dunia ?

Katika  orodha  ya  timu  bora  za  shirikisho  la  kandanda  duniani  FIFA , mapambano  hay ya  nusu  fainali  hayalingani.

Ubelgiji iko  katika  nafasi ya  tatu duniani, Ufaransa  ya  saba, England ya 12  na  Croatia ya 20.

Ufaransa  iliikandika  Ubelgiji  mabao 5-0 mjini  Nantes katika awamu  ya  makundi  mwaka 1984  katika  ubingwa  wa  Ulaya  wakati  Michel Platini alipopachika  mabao 3, na  kisha kushinda  kwa  mabao 4-2  katika  mchezo  wa  nafasi  ya  tatu wa  kombe  la  dunia  mwaka 1986  nchini  Mexico  baada  ya  Ubelgiji kushindwa  katika  nusu  fainali  na  Argentina  kwa mabao 2-0, ambapo Diego Maradona  alipachika  mabao 2.

Kizazi  kimoja  hapo  kabla, Emile Veinante alipachika  bao  katika  dakika  ya  mwanzo  ya mchezo ambapo Ufaransa  ilishinda  mabao 3-1 mjini  Paris katika  duru  ya  timu  16 bora katika  fainali  za  kombe  la  dunia  mwaka  1938.

Tangu  kushinda  taji  lake  pekee  katika  uwanja  wa  Wembley mwaka  1966, England ilifika awamu  ya  nusu  fainali  mara  moja  tu, na  kushindwa  na  Ujerumani  ya  magharibi  wakati huo  kwa  mikwaju  ya  penalti  katika  fainali  zilizofanyika  nchini  Italia  mwaka  1990.

Wachezaji wa Croatia wakishangiria baoPicha: Reuters/H. Romero

Nusu fainali

Ufaransa  ilishindwa  katika  nusu  fainali  mwaka  1958  na  1982, ilishinda  kombe  lake  la kwanza  na la pekee  hadi  sasa  nyumbani  mwaka  1998, na  kisha  kushindwa  katika fainali  mwaka  2006, dhidi  ya  Italia  katika  tukio lililokuja  kuwa  maarufu  ambapo Zinedine Zidane  alimpiga  kichwa  mchezaji  wa  Italia Mataranzzi.

Croatia  ilishindwa  na  Ufaransa  katika  nusu  fainali  za  mwaka 1998  katika fainali  zake za  kwanza  kwa  nchi  hiyo  tangu  kuwa  taifa  huru  baada  ya  kuvunjika  kwa  Yugoslavia.

Kikosi  cha  England kinamjumuisha mtu mwenye  jina  la  utani . Jamie Vardy anamuita mchezaji  wa  timu  ya  taifa  na  timu  ya  Leicester City  Harry Maguire kuwa  ni kichwa pande , Slab head.

vardy alijiunga  na  waandishi  habari  na  kuulizwa swali  la  mwisho. Jamie Vardy kutoka katika  Vardy Express. Kichwa  chako  ni  kikubwa  kiasi  gani?

Kylian Mbappe wa Ufaransa (kulia)Picha: picture-alliance/dpa/M.Bogodvid

Wakati Maguire  alipofunga  bao la  kwanza  katika  ushindi  wa  mabao 2-0 siku  ya Jumamosi dhidi  ya  Sweden, kelele  zake  za  furaha  zilikuwa kali  sana  na  zilionekana kama  anapiga  keleza  za  kuumia.

Msjhambuliaji  wa  Ubelgiji Romelu Lukaku alipata  jina  la  utani  akiwa  Manchester  United, ambako wachezaji  wenzake walifananisha  kazi yake uwanjani  na Sylvester

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW