1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu zote nne za Tanzania zatamba kimataifa

27 Oktoba 2025

Kwa mara ya kwanza katika historia ya soka la Tanzania, taifa hilo limefanikiwa kupeleka timu nne katika hatua ya makundi ya michuano mikubwa barani Afrika chini ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Tanzania | Simba Sports Club
Kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba Picha: Mhindi Joseph

Kwa mara ya kwanza katika historia ya soka la Tanzania, taifa hilo limefanikiwa kupeleka timu nne katika hatua ya makundi ya michuano mikubwa barani Afrika chini ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Baada ya ushindi wa Jumla wa mabao 3-0 dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini, Simba SC imepiga hatua na kuungana na watani wao wa jadi Yanga SC katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika .

Wakati huo huo, upande wa Kombe la Shirikisho Afrika  vilabu vya Azam FC na Singida Black Stars vimeonyesha ukomavu wa hali ya juu kwa kuibuka na ushindi unaowaweka kwenye hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia ya vilabu hivyo.

Katika mahojiano na Mchambuzi wa Soka Jacob Mlay anataja Mafanikio haya ni ishara ya  ukuaji wa soka la Tanzania.

Kikosi cha Yanga SCPicha: Mhindi Joseph

“Timu zote Nne zilizoshiriki Nadhani ni kutokana na uwekezaji ambao kimsingi umefanyika haijaja kwa bahati mbaya itazame  Klabu ya Simba na Yanga mara zote wamekuwa wakifanya hivyo unaona unapata picha uwekezaji wa Simba na Yanga umeshakuwa Mkubwa ndio maanaYanga wameshafika Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Africa Simba pia wamefanya hivyo msimu uliopita wamecheza Fainali kwa hiyo sina mashaka na hivi Vilabu Klabu za Azam FC na Singida Black Stars zimefanikiwa kufika hapa kwa kutokana na  Uwekezaji “Amesema Mchambuzi wa Soka Jacob Mlay

Kwa sasa, macho yote ya mashabiki yameelekezwa kwenye droo za hatua ya makundi, huku Watanzania wakiwa na matumaini kuona timu hizi zikiendelea kutamba na kuleta heshima zaidi kwa taifa.

Ligi ya NBC kuendelea wiki hii

Kwa upande mwingine, Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inaendelea kutimua viwanja wiki hii huku macho ya mashabiki yakiwa yameelekezwa kwa vigogo wawili wa soka Yanga SC naSimba SC  ambao wote wanarejea uwanjani kwa michezo muhimu katikati ya wiki

Kesho Jumanne, tarehe 28 Oktoba katika uwanja wa Benjamin Mkapa unatarajiwa kushuhudia mtanange mkali Mabingwa watetezi Yanga watawakaribisha wakatamiwa Mtibwa Sugar.

Kuhusu Maandalizi Kocha wa Mtibwa Sugar Awadh Juma anasema.

Mashabiki wa Yanga nchini TanzaniaPicha: Mhindi Joseph

“Mpaka saivi tupo na afya njema upande wa Benchi Tunashukuru kila mmoja yupo vizuri na tupo tayari kwa mchezo  ya kesho dhidi ya Yanga “Amesema Kocha wa Mtibwa Sugar Awadh Juma

Kwa upande wa Yanga Mchezaji Offen Chikola“Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wa Kesho hakika haitakuwa mechi Rahisi”Amesema Mchezaji wa Yanga Offen Chikola

Oktoba 30 itakuwa zamu ya Simba SC kuonesha ubabe wao wakiwa nyumbani dhidi ya TRA  United.

Golikipa wa Simba Yakub Suleiman na Mchezaji wa Simba Awesu Awesu kuelekea mchezo huo wanasema.

"Mechi itakuwa Ngumu kwa sababu mechi za ligi hatutaki kupoteza mchezo hata moja kwa hiyo itakuwa mechi ngumu”Amesema  Mchezaji wa Simba Awesu Awesu

“Mchezo unaokuja mashabiki waje kwa wingi kwa uwezo wake Mungu alama tatu lazima tutazipata “Amesema Golikipa wa Simba Yakub Suleiman