1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tofali za tope biashara kubwa vijiji vya Kenya

Veronica Natalis
26 Aprili 2018

Utengenezaji na uuzaji wa tofali za udongo umejitokeza kuwa mkombozi wa wakazi wa maeneo ya vijijini nchini Kenya, wanaozitumia kwaajili ya kujiingizia kipato, na zinasaidia pia kudhibiti hali ya hewa ndani ya nyumba.

Fotowettbewerb KLICK
Picha: Ahmad Al-Bazz

Katika kijiji cha Kivoo mashariki mwa Kenya, Erastus Njiru hutumia njia ya uvuvi wa matope kutengeneza matofali. "Ninaweza kuuza hadi matofali elfu thelathini kwa siku”. Alisema Erastus Njiru mwenye umri wa miaka 34, wakati akisafisha mikono yake iliyokuwa na tope na baadaye kuikausha kwa kutumia taulo.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari wa shirika la habari la Reuters Erastus anasema, tofali moja linauzwa kwa shilingi nane za Kenya na kama biashara ikiwa nzuri anaweza kupata shilingi elfu ishirini na nne za Kenya kwa juma moja. 

Erastus Njiru ni miongoni mwa wakenya wengi wanaouza na kununua matofali ya tope kwa ajili ya kujengea nyumba ambazo ni za gharama nafuu na zinazoendana na mazingira ikilinganishwa na nyumba zinazojengwa kwa mawe au matofali ya saruji.

Nyumba za tofali za tope zinadhibiti baridi na joto ndani ya nyumba.Picha: Ahmad Al-Bazz

Nyumba zaidi zajengwa kwa tofali za udongo

Takribani asilimia 15 ya nyumba mpya kwa sasa zimejengwa na matofali ya tope, ikilinganishwa na asilimia moja ya mwaka 2010 na hiyo ni sawa na kusema kuna ongezeko la asilimia kumi na nne ya nyumba za matofali ya udongo kwa kipindi cha miaka minane tangu mwaka 2010, na hiyo ni kwa mujibu wa afisa mkuu katika wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya mijini, Aidah Munano.

Mahitaji ya matofali ya tope kwa Kenya yapo katika maeneo ya vijijini zaidi kwa sababu nyumba zilizojengwa kwa matofali hayo zinaweza kutoa baridi wakati wa joto na kutoa joto wakati wa usiku, na gharama yake ni nusu ya ile ya matofali yaliyotengenezwa kwa saruji au mawe. Hiyo ni kwa mujibu wa Gitonga Murungi, muhifadhi kutoka Kenya.

Inaelezwa kuwa watu wa maeneo hasa ya vijijini nchini Kenya wanaogopa kujenga nyumba zao kwa kutumia mawe kwa gharama kubwa ikilinganishwa na matofali ya tope. 

Utengenezaji wa tofali za tope umekuwa chanzo cha mapato kwa Wakenya wengi waishio katika maeneo ya vijini.Picha: Reuters/N. Chitrakar

Chanzo cha ada ya watoto

Mmoja kati ya wakulima wa zamani nchini Kenya anasema kuwa yeye hakupata nafasi ya kumaliza masomo yake ya shule ya sekondari kwa sababu ya kukosekana kwa pesa za kulipa ada ya shule, lakini kwa sasa yeye anaweza kumudu gharama za kuwasomesha watoto wake mpaka chuo kikuu kwa biashara hiyo ya kuuza matofali ya tope.

Ayubu Shaka, mkurugenzi msaidizi wa idara ya hali ya hewa Kenya amesema kuwa upepo mkali sana katika nchi ya Kenya ni kitisho kwa raia kwa sababu mazao na mifugo wanapotea kwa kukosekana kwa maji.

Kuongezeka kwa joto kumemsababisha Milka Njeri mkulima wa mtama nchini humo kuzingatia utengenezaji wa matofali kama chanzo kingine cha mapato ya ziada. Anasema hapati pesa nyingi lakini si haba kwani anaweza kupata shilingi 2000 za Kenya kwa juma moja.

Watengenezaji wa matofali ya tope wanashauriwa kuhakikisha kuwa kazi yao haiharibu mazingira alisema Violet Matiru mhifadhi katik ashirika la misaada linalojihusisha na kutoa eleimu kuhusu masuala ya mazingira.

 

Mwandishi: Veronica Natalis/ Reuters

Mhariri: Josephat Charo