1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOFAUTI KATI KANZLER SCHRÖDER NA WAZIRI WA NJE FISCHER JUU YA CHINA

6 Aprili 2005

Kuhusu msimamo wa waziri wa nje wa Ujerumani Joshka Fischer juu ya marufuku ya silaha kwa China, gazeti la kibiashara linalochapishwa mjini Düsseldorf laandika:

"Kanzela Schröder anajikuta pekee yake katika swali iwapo UU uondoshe marufuku yake ya silaha au la.Baada ya vikundi vya wabunge wa vyama-tawala kile cha SPD na KIJANI,sasa pia waziri wa nje Joshka Fischer ameelezea hadharani shak shaka zake juu ya busara ya kuondoa marufuku hayo.Amekisia kwamba gharama ya kuchukua hatua hiyo ni kubwa mno katika usuhuba kati ya Ulaya na Marekani.Kwahivyo, swali linazuka –kwanini Kanzela Schröder anan’gan’gania msimamo wake huo ?"-lauliza HANDELSBLATT.

Gazeti la Magdeburg VOLKSTIMME linaona kumeibuka changamoto kati ya Kanuzela na waziri wake wa mambo ya nje:Linaandika,

"Fischer na Schröder hawashindani bega kwa bega bali wanapapurana uso kwa uso.Wanagombana kuhusu China na marufuku ya silaha iliowekewa China.

Kanzela Schröder amesema hata ikiwa Bunge halitaidhinisha ataiuzia China silaha.Waziri wake wa nje haafiki mpango huo.Schröder anahisi China ya leo ni tofauti na ile ya mwaka 1989-mwaka ambao vifaru vyake vilitawanya waandamanaji katika uwanja wa Tianamen mjini Beijing.

Bw.Fischer yabainika ametiwa shindo na chama chake ili kuchukua msimamo tofauti."-laandika gazeti.

Ama Gazeti la NEUE WESTFÄLISCHE kutoka Bielefeld laandika:

"Tofauti zimeibuka kuhusu China.Shina la wapigakura wa chama-tawala cha SPD si la kutarajia kuungamkono biashara ya silaha nchi za je.Na waziri wa nje Fischer anaelewa hayo.Endapo Kanzela Schröder akishikilia uzi wake ule ule,ni chama cha SPD kitakachoadhibiwa na wapigakura wake na sio chama cha Kijani.Kwa jicho hili,mkakati anaoutumia Bw.Fischer hautokani tu na imani ya kisiasa bali pia ni mbinu ya kisiasa."-lasema NEUEWESTFÄLISCHE kutoka Bielefeld.

Katika gazeti la LANDESZEITUNG linalochapishwa Lüneburg tunasoma:

"rai ya Kanzela Schröder ya kutaka kuiuzia China silaha imekuja kama kiokozi cha mdundo wa kuashiria mapumziko.Msimamo mkali na wa

kiadilifu usioregarega mbele ya wenyedhamana ya mauaji ya Tianamenplatz unawavutia alao shina la wafuasi wa chama cha Kijani cha walinzi wa mazingira.Ili kupangusa madoa yake nchini Ujerumani,anapaswa kumtafuta adui mwengine."Lausia gazeti.

Gazeti la WETZLARER NEUE ZEITUNG laandika:

"Katika mvutano kati ya kuonesha utiifu kwa Kanzela au chama ,waziri wa nje Fischer hana chaguo bali kushikamana na msimamo wa chama chake.Hivyo kupinga kuuziwa silaha china.lakini lazuka hapo swali:kwanini anachukua msimamo huo sasa ? Inabainika dhahiri shahiri kwamba waziri huyu anaependa vyombo vya habari, sasa anapotelewa na hisia.

Likitugeuzia mada, gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG lachambua uwezekano wa wastaafu mwaka huu kuondokea bila ya nyongeza za malipo yao ya uzeeni.

Laandika kwamba, mfumo mpya wa malipo ya wastaafu ulipaswa kulenga kwamba malipo ya uzeeni hayaongezeki kwa kima kikubwa zaidi kupita cha wafanyikazi ili mfumo wa bima ufanye kazi.Kutokana na kifungu cha daraja ya kupanda malipo hayo, yanabidi sasa kubaki chini.sasa ikiwa serikali haidhamiri kuwadanganya wapigakra juu ya makisio yamalipo kwa kipindi kijacho,itapaswa kukifuta kifungu hicho au alao kupunguza athari zake.Hii maana yake kwa wastaafu:sio hawapati nyongeza kabisa,bali wanapunguziwa hata kima wapatacho sasa.

Mwishoe, gazeti la NEUES DEUTSCHLAND laandika:

"......Tangu serikali ya chama cha SPD na ya KIJANI na hata itakayoongozwa na vyama vya Upinzani,zote zitawapokonya fedha wastaafu.

Kutokana na matokeo haya mengi ya aina hii,ndipo sasa hakuna aneshughulishwa na siasa au uchumi........"

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW