1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Tabia NchiAzerbaijan

Tofauti zaibuka katika mkutano wa COP29

13 Novemba 2024

Viongozi wa dunia wanatofautiana juu ya njia za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Mkutano wa COP29, 2024 | Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev
Ripoti mpya imetoa wito kwa dunia kufikia lengo la kuondosha kabisa hewa ya kaboni mapema zaidi kuliko ilivyopangwa.Picha: Sean Gallup/Getty Images

Tofauti hizo zimejitokeza kwenye mkutano wao unaoongozwa na Umoja wa Mataifa unaoendelea nchini Azerbaijan.

Hayo yanajiri wakati ambapo ripoti mpya inatoa wito kwa dunia kuitaka ifikie lengo la kuondosha kabisa hewa ya kaboni mapema zaidi kuliko ilivyopangwa.

Ripoti hiyo imetolewa kwa viongozi hao wanaokutana nchini Azerbaijan kwa ajili ya mkutano wa  COP29, kujadili lengo la kufikia makubaliano juu ya kuongeza fedha ili kuyasaidia mataifa yanayoendelea kukabiliana na majanga ya hali ya hewa na pia kugharamia mchakato wa kuhamia kwenye nishati safi.

Kulingana na ripoti hiyo, ili kufikia lengo kuu la makubaliano ya Paris la kupunguza joto hadi nyuzi joto 1.5, dunia sasa ingehitaji kufikia hatua ya kuondosha kabisa, hewa chafu hadi ifikapo mwishoni mwa miaka ya 2030 badala ya miaka ya 2050

Nchi zinazoendelea zinazitaka nchi tajiri zitenge kiasi cha dola trilioni 1.3 kila mwaka kwa ajili ya kuzisaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.