Togo inazingatia kujiunga muungano wa kiusalama wa Sahel
17 Januari 2025Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo Robert Dussey amesema taifa hilo halijakataa kujiunga na mkataba wa ulinzi wa Saheluliobuniwa na serikali zinazoongozwa na jeshi za Burkina Faso, Mali na Niger.
Dussey amesema kwenye mahojiano na kituo cha Voxafrica alipoulizwa ikiwa taifa hilo litajiunga na mkataba huo wa AES, kwamba inategemeana na uamuzi wa rais.
Viongozi wa Burkina Faso, Mali na Niger waliunda AES baada ya kuchukua mamlaka kufuatia mapinduzi ya kati ya mwaka 2020 na 2023 na kujiengua kwenye Jumuiya ya Kiuchumi kwa mataifa ya Magharibi, ECOWAS.
Ikiwa Togo itajiunga, mataifa hayo matatu yasiyo na bandari yataweza kuufikia mji mkuu wa Togo na bandari ya Lome kwa ajili ya biashara.