Togo yasogeza mbele uchaguzi wa bunge
10 Aprili 2024Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sababu ya kuahirishwa uchaguzi huo ni kutowa nafasi ya majadliano zaidi juu ya mageuzi yanayohitajika kufanyika kwenye katiba, hatua ambayo wapinzani wanasema ni mbinu ya kumpa nafasi Rais Faure Gnassibe kuendelea kusalia madarakani.
Upinzani Togo waitisha maandamano kupinga kuahirishwa uchaguzi wa Bunge
Kiongozi huyo ametawala tangu mwaka 2005 baada ya kumrithi baba yake, ambaye naye alikuwa ametawala kwa zaidi ya miongo mitatu.
Tamko la jana la serikali lilitoka siku chache kabla ya maandamano makubwa yaliyopangwa kufanywa na vyama vya upinzani.