TOKYO. Ajali ya garimoshi yaua watu 50 nchini Japan.
25 Aprili 2005Matangazo
Watu wasiopungua 50 wameuwawa na wengine zaidi ya 200 wakajeruhiwa katika ajali ya garimoshi la abiria nchini Japan. Garimoshi hilo liliwacha reli na kuanguka baada ya kuigonga motokaa iliyokuwa ikivuka reli hiyo, kilomita 400 magharibi mwa mji wa Tokyo. Maafisa wa serikali wanasema uchunguzi unafanywa kutathmini chanzo halisi cha ajali hiyo.