1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Chama cha LDP kimeshinda uchaguzi nchini Japani

12 Septemba 2005

Chama tawala cha LDP nchini Japani kimejizolea ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanywa nchini humo.Tarakimu za hadi hivi sasa zinaonyesha kuwa chama tawala kitakuwa na viti 296 katika bunge la viti 480.Kwa mara ya mwanzo tangu miaka 15,chama cha LDP kitakuwa na uwingi bungeni.Chama cha upinzani,Democratic Party kimejipatia viti 113,hiyo ikiwa ni hasara ya kama theluthi moja.Kufuatia matokeo hayo,kiongozi wa chama hicho cha upinzani,Katsuya Okada amejiuzulu akisema kuwa ujumbe wa chama haukufika kwa wananchi.Kwa upande mwingine,waziri mkuu Junichiro Koizumi amesema,matokeo ya uchaguzi yameonyesha kuwa mpango wake wa kutaka kubinafsisha posta ya Japani,unaungwa mkono na wengi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW