1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO-Idadi ya waliokufa katika ajali ya treni yaongezeka.

27 Aprili 2005

Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali mbaya ya treni kuwahi kutokea nchini Japan kwa zaidi ya miaka 40 imeongezeka na kufikia zaidi ya watu 80.

Juhudi za kuwaokoa watu sasa zimeingia katika siku ya tatu,huku polisi wakiwa wanaamini kuna uwezekano wa watu wengine wamenasa katika mabehewa yaliyoharibika.Hata hivyo haijaweza kufahamika mara moja iwapo watu hao wangali hai au wameshakufa.

Zaidi ya watu 400 pia walijeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea juzi siku ya Jumatau,wakati teni hiyo ilipogonga jengo moja baada ya reli kung’oka katika mji wa Amagasaki,kiasi cha kilometa 400 magharibi mwa Tokyo.

Polisi wanaendelea kuchunguza katika ofisi za shirika la reli la JR West kutafuta chanzo cha kung’oka kwa reli.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW