TOKYO: Japan yaanza mazoezi ya kila mwaka ya baharini
23 Oktoba 2006Matangazo
Majeshi ya majini ya Japan yameanza mazoezi yake ya kila mwaka katika mazingira mapya kufuatia kitendo cha jirani yake Korea ya kaskazini kuripuriwa bomu la kinyuklia. Kulingana na ripoti za magazeti, Japan inafikiria ikiwa itatuma manuari za kijeshi katika bahari ya Japan kufuatia kwa karibu utekelezaji wa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Korea ya kaskazini. Japan inafikiria pia kutumia ndege kupeleleza hali ya mambo juu ya anga ya eneo hilo.
Korea ya kaskazini imezituhumu Japan, Marekani na Korea ya kusini kwa uchokozi wa kivita.