1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo. Japan yataka kuombwa radhi kutokana na maandamano yaliyosababisha uharibifu mkubwa wa mali katika ubalozi wake mjini Beijing.

14 Aprili 2005

Waziri wa mambo ya kigeni wa Japan amesema leo kuwa ataitaka China kuacha kile ambacho nchi yake inaamini ni uungaji mkono rasmi wa maandamano dhidi ya nchi yake, wakati wanaharakati wa Kichina wametoa wito wa kufanyika maandamano makubwa zaidi mwishoni mwa wiki hii.

Waziri wa mambo ya kigeni Nobutaka Nachimura anatarajiwa kuwasili mjini Beijing siku ya Jumapili wakati hali ya wasi wasi ikizidi kupanda kati ya nchi mbili hizo jirani, baada ya Japan kuidhinisha kitabu cha historia kitakachotumika mashuleni, pamoja na hatua ya utafutaji wa gesi na mafuta katika maeneo yanayogombaniwa na nchi hizo mbili.

Japan imeitaka China iombe radhi pamoja na kudai fidia kutokana na ghasia za wiki iliyopita, wakati maelfu ya waandamanaji walipoandamana hadi katika ubalozi wa Japan na kurusha mawe na chupa katika maandamano makubwa ambayo hayajawahi kutokea kwa miaka mingi mjini Beijing.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW